Viongozi wa huduma ya Good for all ministries kwa kushirikiana na dini,na madhehebu mbalimbali walisafirio hadi mtera Mtera kwa ajili ya kumuomba MUNGU alete mvua itakayosaidia upatikanaji wa maji katika mabwawa yetu hasa katika mikoa ya nyanda za juu .kusini,mikoa ya Iringa,na mbeya na kanda ya kati yaani Dodoma na Singida,maeneo ambayo kwa kiasi kukubwa ndiyo yanayonywesha Bwawa la Mtera.pia aliotoa pole kwa watanzania waliopata ajali ya meli ya islandermaeneo ya nungwi ,ajali ya basi la championi huko Dodoma,na ajali ya mvua ya kimbunga huko mbagala ambapo zaidi ya nyumba 104 ziliezuliwa mapaa na kuharibiwa,alisema askofu huyo”.
Pia alisema kutokana na utafiti wa kiroho walioufanya imeonyesha kuna watu wanatumia nguvu za giza kuzuia mvua kwa maslahi yao binafsi, kwa uchawi, au kwa laana ,au kwa uganga na kwa matambiko,pia aliongeza kwamba watu hao wananufaika sana kwa kukosekana kwa mvua katika nchi pasipo kujali shida wanayoipata wananchiwalio wengi alisema Askofu Gadi.”
Pia aliongeza kuwa wanatoa masaa 72 kw wote wanaofanya shughuli za kutumia nguvu za giza waache mara moja, la sivyo sheria ya kiroho itachukua mkiondo wake,siku ile ambayo tuta fanya maobi maalumu siku ya tarehe 6.mwezi wa kumi.mwaka 2011 Biafra saa 4.00asubuhi vile vile walialika watu wa dini mbalimbali na madhehebu mbalimbali kuombea Taifa letu na kupambana na nguvu za Giza zinazozuia mvuaa isinyeshe katika nchi yetu.
Leave a Reply