Feeds:
Posts
Comments

Waziri wa maendeleo ya makazi Bi. Anna Tibaijuka juzi alizindua mradi wa nyumba za wana Federation huko Chamazi, mpango huo ulianza mwaka 2004  katika wilaya ya Temeke na kuasisiwa na shirika la centre for all community Initiative (CCI).mnamo mwaka  2005 vikundi vingine vilianzishwa mkoani Arusha,Dodoma,na Musoma.Hivi sasa kuna vikundi 175 vyenye wanachama 7500 ambavyo kwa pamoja vina akiba ya zaidi ya milioni 1i6 na mfuko wa jenga na milioni 25.

Federation ni muungano wa mtandao wa vikundi mbali mbali vya kijamii hususani akina mama,vilivyoamua vyenyewe kuweka akiba ya kila siku kwa lengo la kuondoa umaskini.mpango huo ni wa kimataifa ambao unahusisha nchi za 20 duniani ambazo ziko Afrika,Asia  na Amerika ya Kusini.

Muungano huu unasaidiwa na shirika la centre for community Initiative(CCI) ambalo ni sehemu ya shirika la slum Dwellers international (SDI),mradi huo umewezesha kujenga uwezo wa jamii(federation kufanya utafiti wa maeneo yao hususani kurasini kwa lengo la kujitambua na kuchukua hatua ya maendeleo.

“Pia walisema Taasisi zilizochangia mradi huu ni UNHABITAT,SDI,HomelessInternation,Wizara ya Ardhi,na manispaa ya Temeke.pia changamoto zinazokabili ujenzi wa nyumba za gharama nafuu nim kama ukosefu wa ardhi yenye gharama nafuu kwa watu wernye kipato cha chini hali inayopelekea wakazi wengi kuendelea kuishi katika makazi holela,ukosefu wa sera ya kuhamishwa watu katika makazi (resttlement policy)hupelekea uhamishwaji kufanyika bila utaratibu maalumu. walisema wana mradi huo”.

Hata hivyo walisema ukosefu wa vyombo vya kifedha vinanyotoa mikopo ya nyumba ya gharama nafuu,pia tatizo la miundo mbinu katika makazi kama barabara,maji,mfumo mwamaji taka  na umeme vitu ambavyo nimeonekana kuwa  tatizo kwa wanachi.

 

 

Advertisements

Viongozi wa huduma ya Good for all ministries kwa kushirikiana na dini,na madhehebu mbalimbali walisafirio hadi mtera Mtera kwa ajili ya kumuomba MUNGU alete mvua itakayosaidia  upatikanaji wa maji katika mabwawa yetu hasa katika mikoa ya nyanda za juu .kusini,mikoa ya Iringa,na mbeya na kanda ya kati yaani Dodoma na Singida,maeneo ambayo kwa kiasi kukubwa ndiyo yanayonywesha Bwawa la Mtera.pia aliotoa pole kwa watanzania waliopata ajali ya meli ya islandermaeneo ya nungwi ,ajali ya basi la championi huko Dodoma,na ajali ya mvua ya kimbunga huko mbagala ambapo zaidi ya nyumba 104 ziliezuliwa mapaa na kuharibiwa,alisema askofu huyo”.

Pia alisema kutokana na utafiti wa kiroho walioufanya imeonyesha kuna watu wanatumia nguvu za giza kuzuia mvua kwa maslahi yao binafsi, kwa uchawi, au kwa laana ,au kwa uganga na kwa matambiko,pia aliongeza kwamba watu hao wananufaika sana kwa kukosekana kwa mvua katika nchi pasipo kujali shida wanayoipata wananchiwalio wengi alisema Askofu Gadi.”

Pia aliongeza kuwa wanatoa masaa 72 kw wote wanaofanya shughuli za kutumia nguvu za giza waache mara moja, la sivyo sheria ya kiroho itachukua mkiondo wake,siku ile ambayo tuta fanya maobi maalumu siku ya tarehe 6.mwezi wa kumi.mwaka 2011 Biafra saa 4.00asubuhi vile vile walialika watu wa dini mbalimbali na madhehebu mbalimbali kuombea Taifa letu na kupambana na nguvu za Giza  zinazozuia mvuaa isinyeshe katika nchi yetu.

Ukame watishia Somalia.

Kulingana na Umoja wa Mataifa hali ya ukame inayoshuhudiwa nchini Somalia ni mbaya zaidi katika kipindi cha miaka 50.

Wakati huo huo Umoja wa Mataifa umesema kuwa mashirika ya kutoa misaada yanahitaji kupata hakikisho zaidi kutoka makundi ya wapiganaji hasaa wale wa Al shabaab kabla kupeleka misaada nchini humo.

Kundi la Al shabaab ambalo lina uhusiano na lile la magaidi la Al Qaeda lilikuwa limewekea mashirika hayo marufuku ya kufanya kazi katika maeneo ya kusini mwa Somalia. Hata hivyo marufuku hiyo iliondolewa wiki iliopita.

Na shirika la Oxfam limelalamika kuwa wafadhili wamelegea katika kuchangia misaada kusaidia walioathirika na ukame katika upembe wa Afrika.

Shirika hilo limesema kati ya dola bilioni moja zinazohitajika, kufikia sasa ni dola milioni 200 zilizokusanywa kufikia sasa.

Shirika  limewataka wafadhili waitikie mwito huo  kuzuia hali kuwa mbaya zaidi.

Huku, harakati za kuwashawishi wafadhili watoe michango yao, raia wa Somalia wanaofanya biashara nchini Kenya na ng’ambo, wameanza  harakati za kuchangisha pesa na vyakula kusaidia wenzao.

mwenyekiti wa kundi hilo Hassan Guled hajaweka wazi wamechangisha kiwango kipi cha pesa na ni misaada kiasi gani imekusanywa amesema mikakati inafanywa kuanza kusafirisha vitu vilivyopatikana hadi kwenye mpaka wa Kenya na Somalia walipo wakimbizi hao.

Spika wa Bunge mhe.Anna Makinda wakimkumbuka mke wa mbunge khamis Silima aliyefariki Dunia kwa ajali eneo la nzuguni mkoani Dodoma.(picha kwa hisani ya new habari)

MBUNGE wa Baraza la Wawakilishi  wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Mussa Khamis Silima amefiwa na mkewe baada ya gari alilokuwa akisafiri nalo kupata ajali likitokea Morogoro kuja mjini Dodoma.

Akizungumzia tukio hilo jana bungeni , Spika Anne Makinda alilitaarifu Bunge kuwa ajali hiyo iliyosababisha kifo ilitokea juzi majira ya saa 1:45 usiku eneo la Nzuguni katika Mkoani ya Dodoma.

Bunge jana lililazimika kukaa kimya kwa dakika moja likikumbuka msiba huo kabla ya kuendelea na shughuli nyingine za bunge, mara baada ya Makinda kutoa tangazo hilo bungeni.

“Waheshimiwa Wabunge naomba nitamke kwa masikitiko makubwa kuwa jana Agosti 21 saa mbili kasorobo katika eneo la Nzuguni, mheshiwa Mussa Silima akiwa na msafara na familia yake walipata ajali na katika ajali hiyo mke wa Mbunge alifariki, naomba tusimame kwa dakika moja kumkumbuka,” alisema Makinda.

Alisema Marehemu, Mwanaheri Twalib ambaye mwili wake ulisafirishwa jana kwa ndege ambayo pia ilimbeba mumewe (mbunge) na dereva wake kwa ajili ya kupelekwa jijini Dar es Salaam kwa matibabu, anatarajia kuzikwa kwao baada ya taratibu kukamilika.

Akielezea  zaidi, Makinda alisema ajali hiyo imetokea wakati mbunge huyo akitokea Zanzibar, ambako walikwenda kumzika Kaka wa marehemu mkwewe na walikuwa wakirejea kuwahi vikao vya bunge vilivyokuwa vikiendelea Dodoma.

Wakina mama 21 wameripotiwa kufariki dunia katika wilaya ya Tunduru  mkoani Ruvuma  baada ya kile kilichoripotiwa kuwa ni uzembe wa kutozingatia ushauri wanaopewa na wataaalamu wa afya katika vituo mbalimbali vya afya vikiwemo zahanati,vituo vya afya mkoani humo kawa utafiti uliofanyika tangu mwaka 2000 mpaka 2011 imeonyesha wanawake wanaliofariki imefdikia idadi hiyo.

Kwa mujibu wa maelezo ya Daktari Chiwangu alisema” vifo hivyo vimesababaishwa na ukaidi wa wajawazito hao kutofuata alamaza hatari”mwisho wa kumnukuu pia inasemekana wajawazito hao husubiri mpaka wawe wameshikwa na uchungu hali inayowapelekea kupata maumivu makali kabla ya kufikishwa jkatika vituo vya afya au hospitalini au kataika zahanati husika.

Vifo vya akina mama hao husababishwa na kutembea kwa umbali mrefu hali inayowasabaishia wengine kujifungulia njiani na wengine kufarijki kwa kukosa msaada wa wataalalmu wa afya ambao kwa wakati huo huwa mbalina eneo la tukio ambalo mama mjamzito anakuwa amekumbwa na mkasa.

Hata hivyo daktari huyo amewaasa akinamama wajawazito kufuata maelekezo wanayopewa na wataa;amu wa afya na kuacha kuwa wakaadi hali ambayo inawapelekea  matatizo na hata vifo.

kikongwe mmoja ambaye  hakutambulikana mara moja alikutwa amekufa kwa kuchomwa moto wilayani mbozi kwa kile kilichojulikana kwamba ni mchawi na alikuwa akishukiwa kwa baadhi ya matukio mbalimbali kijijini hapo, hata hivyo watuhumiwa waliofanya uhalifu huo walitokomea pasipojulikana baada ya kitendo hicho.

Jeshi la polisi mkoani hapo linaendelea na upelelezi wa kipolisi  pamoja na kuwasaka watuhumiwa wa mauaji hayo mpaka tunaondaka eneo la tukio nyumba ya marehemu ilikuwa imechomwa kwa moto na kuteketezwa kwa mali za marehemu.

mhariri mwakiteleko

Wahariri wakitoa jeneza lenye mwili wa aliyekuwa kaimu Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New habari 2006 na Mhariri wa Rai,Daniel Daimon Mwakiteleko nyumbani kwake Tabata Chango’mbe kata ya segerea jijini Dar es salaam jana kwa ajili ya kusafirishwa kwenda Mwakaleli Wilaya ya Rungwe kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika leo.